Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza ofisini kwake na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani Majola (katikati). Ziara hiyo, ambayo pia ilikuwa na lengo la msajili huyo kujitambulisha na kumsalimia Waziri Nchimbi, na kumuelezea shughuli mbalimbali zifanywazo na mahakama hiyo pamoja na kumuelezea changamoto mbalimbali zinazoikabili mahakama hiyo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliahidi kushirikiana na mahakama wakati wowote itakapohitaji msaada kutoka ofisini kwake.
Msajili
wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Bongani
Majola (katikati) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (kushoto) kuhusiana na mafanikio na changamoto
mbalimbali ya Mahakama hiyo ambayo Makao Makuu yake yapo jijini Arusha.
Kulia ni Msemaji wa Mahakama hiyo, Roland Amoussouga.
Msemaji
wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Roland
Amoussouga akimfafanulia masuala mbalimbali Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) wakati viongozi hao walipomtembelea
waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kutoka
kushoto ni Msajili wa Mahakama hiyo, Bongani Majola. Kulia ni
Mwanasheria wa mahakama hiyo, Jerry Mburi.

No comments:
Post a Comment