HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 18, 2013

MRISHO MPOTO ( MJOMBA) AONESHA TOFAUTI KUBWA KATIKA TASNIA YA MICHEZO YA KUIGIZA YA JUKWAANI

Pichani ni kusho ni Bw, Mrisho Mpoto akiigiza kama FALSTAFF na kulia ni Bw Ogutu Mulaya, alie tafasiri mchezo huu kwa Kiswahili, akicheza kama Bi Quickly.
Pichani katikati ni Bw Mrisho Mpoto akiwa na waigizaji wenzake kutoka Kenya ambao waliigiza kama WANAWAKE WA HERI WA WINSA wakionesha umahiri wao katika Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Pichi Kulia kabisa ni Bw Ogutu Mulaya, alie tafasiri mchezo huo kwa Kiswahili, akiigiza na wenzake huku akuwa kwenye husika nyingine.

NA SIXMUD J. BEGASHE wa Makumbusho ya Taifa.

Mrisho Mpoto ni moja kati ya wasanii wakubwa wa Muziki na Maigizo ya Jukwani hapa nchini. Michezo hii ya jukwaani ambayo ni adimu na adhimu hapa nchini kutokana na umanikini na utaalaam mkubwa unao hitajika katika uandishi, uongozaji na hata uchezaji jukwaani.

Hapa nchini kuna wasanii wachache wenye uwezo wa kutimiza hatua zote za maandalizi ya mchezo wa jukwaani. Tumekuwa tukishuhudia wataama walio pikwa kutoka Taasisi ya Sanaa, Utamaduni Bagamoyo na wale wa Chuo kikuu cha Mlimani katika Idara ya Sanaa na Maonesho na Chuo kikuu Huria wakishughulika sana na tasnia hii.

Baada ya kuona Tasnia hii inasua sua, Bwana Mrisho Mpoto aliamua kwa dhati kurudisha heshma ya michezo hiyo kwa kuishawishi kampuni inayo jishughulisha na Maonesho ya Jukwaani ya nchini Kenya Kuuleta mchezo ulio jipatia umaarufu mkubwa kwenye nchi mbali mbali ulimwenguni na hata kupata heshma ya nyota tano nchini Uingereza ambapo Mrisho yeyemwenyewe akiucheza mchezo huo kama muhusika mkuu.

Kutokana na kukubali kwa kampuni hiyo Bwana Mrisho aliwashirikisha wadau wapenda maendeleo ya sanaa mchini, Clouds FM na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam ambao ndio walitoa mchango mkubwa wa kufanikisha onesho hilo lifanyikie hapa nchini.

Mwishoni mwa wiki hii Onesho hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na kuudhuriwa na watazamaji wengi wanao elewa umuhimu wa michezo ya jukwaani.

Watazamaji walisifia Umahiri ulio oneshwa na Mrisho Mpoto na waigizaji wengine ambapo waliwafanya watazamaji kutabasamu kwa furaha kubwa kila wakati wa mchezo huo.

Baadi ya washabiki walisema kuwa, wameshangwaza sana kwa kuona kuwa wasanii wafilam hapa nchini hawajajitokeza kabisa kuja kushuhudia uzuri wa sanaa za jukwaani, kwani kwa kufanya hivyo wangeweza kujifunza uigizaji wa kweli, na unao hitaji umakini na taalam wa kutosha toshauti na michezo ya filam inayo ibuka sasa kila kukicha. Wametoa wito kwa watanzania na wasanii wote nchini kuwa na tabia ya kushiriki katika maonesho mbali mbali hapa nchini yenye sura ya kuelimisha kwakupitia utamaduni wetu.

Nae mmoja wa wasanii kutoka Kenya ambae hakupenda jina lake litaje alisema kuwa, wamependezwa na kufurahishwa sana na jitihada za msanii Mrisho Mpoto anazo zionesha pindi anapo kuwa mazoezini na kisha jukwaani, na ameto wito kwa wasanii mbali mbali Tanzania kufuata nyao za Msanii huyu katika harakati zake za jurejesha heshma ya Michezo ya jukwaani kwani ndio inae weza udhuriwa na wanafamilia tofauti na sanaa zingine ambazo ni maarufu kwa sasa.

Akitoa shukrani zake baada ya onesho Bw, Mpoto alimshukuru sana Mkurugenzi wa Cloud Media Bw Ruge Mtahaba kwa kukubali kuisaidia tasnia ya Michezo ya kuigiza ya Jukwaani. Ili kurudisha heshma ya michezo hiyo hapa nchini, pia Bw Mpoto aliushukuru Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa kukubali kutoa mchango wake mkubwa katika kufanikisha onesho hilo na kuonesha moyo wa kuendelea kusaidia wasanii hapa nchini katika kuinua na kuendeleza Utamaduni wa Mtanzania.

Mchezo wa Wanawake wa Heri wa Winsa uliotokana na kitabu kitabu kilicho andikwa na Shakespeare takribani miaka 1600 iliyo pita, na kutafasiriwa na Bw Ogutu Mulaya wa nchini Kenya, ulishirikisha waigizaji nane ambapo kila mwigizaji alifaa husika zaidi ya tatu, na wote walizimudu vyema husika hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad