Mwenyekiti
wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila Kairuki
akisoma hotuba katika maadhimisho ya miaka 14 ya Kumbukumbu ya siku ya
Muasisi wa Shirika Hayati Prof. Hubert Kairuki. Alisema kuwa Tangu
Muasisi huyo amefariki Februari 6, 1999, shirika lao limejiwekea
utaratibu wa kumuenzi kwa kutenda yale mambo muhimu aliyokuwa
akiyathamini wakati wa uhai wake.
Hayati Prof. Hubert
Kairuki alithamini jitihada za serikali na mashirika yasiyo ya
kiserikali ya kuongeza idadi ya rasilimali watu kwenye fani za udaktari
na uuguzi katika sekta ya afya. Ni katika jitihada hizo ndiyo aliamua
kutoa mchango wake kwa kuanzisha shule ya Wauguzi ya Mikocheni
(Mikocheni School of Nursing) na baadae kuanzisha Chuo Kikuu cha Tiba.
Aliongeza
katika maadhimisho ya kumuenzi mwasisi huyo, shirika lao kwa mwaka 2013
wameamua kijikita katika mambo matatu; Kutoa elimu ya Afya kwa
wanafunzi wa shule ya msingi Mikocheni. Pili, kutoa zawadi ya madawati
yapatao 50 kwa shule hiyo ya msingi Mikocheni yenye thamani ya shilingi
milioni 4,500,000/=. Tatu, Shirika kupitia chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya
Hubert Kairuki limetayarisha mhadhara kwa jamii 'Public Lecture' ambayo
itatolewa na mwananzuoni Mtaalam Bingwa katika Afya ya jamii Prof.
Theonesta Mutabingwa ambapo umelenga kutoa somo la matibabu ya ugonjwa
wa malaria kwa wanawake wajawazito.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mikocheni wakiimba wimbo kuwakaribisha wageni.
Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila
Kairuki (kushoto) akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuph Mwenda
akiongea machache katika halfa hiyo. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa
Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila
Kairuki.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akitoa shukrani zake.
Wanahabari nao hawakuwa nyuma kunasa tukio.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana akipokea zawadi ya madawati kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila
Kairuk.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Diwani wa Kata ya Mikocheni, Yusuph
Mwenda akitoa shukrani kwa Mwenyekiti
wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila
Kairuki mara baada ya kukabidhi zawadi hizo za madawati.
Wanafunzi wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa kwa madawati hayo.
Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Mikocheni, Bibi Kokushubila
Kairukia akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugombana (kushoto) na

No comments:
Post a Comment