Meneja wa uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi sare za shule Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasibu Pangahela mwishoni mwa wiki hii, akishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii (katikati) bi Hawa Bayumi.
Meneja wa uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kiromo sare za shule zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii,akishuhudia makabidhiano hayo (wa pili kushoto) meneja wa huduma kwa jamii bi Hawa Bayumi akifuatiwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiromo Nasib Pangahela, Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemoKaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki akimvalisha sare za shule na viatu mwananfunzi wa shule ya msingi Kiromo zilizotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel mwishoni mwa wiki hii. Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania Dangio Kaniki (Kulia) akimpongeza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kiromo (kulia) baada ya makabidhiano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii wakishuhudiwa na meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi (wa pili kulia) akifuatiwa na mmoja wa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo bi Zuwena Salumu, Airtel metoa msaada wa sare za shule zikiwemo Kaptura 600 ,skirt 600 , mashati 1193 na viatu 728 vyote vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa gharama nafuu zaidi Tanzania, leo
imegawa sare za shule pamoja viatu katika shule ya msingi Kiromo
iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani, ikiwa ni sehumu ya shughuli zao za
kusaidia jamii.
Shule
ya kiromo ni moja kati ya shule zilizofaidika na mpango wa shule yetu
na kuingia kwenye ukarabati wa majengo na madarasa na kubadili mazingira
ya shule na kutoa vifaa vya kufundishia pamoja na computer. sasa Airtel
imetoa Sare na viatu vya shule kwa wanafunzi wote shuleni hapo.
Katika
kauli iliyotoleawa na kampuni ya Airtel Tanzania kupitia Meneja
shughuli za kijamii bi. Hawa Bayumi alisema” Airtel imedhamiria
kuendelea kuisadia shule mbalimbali kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwepo
vya kufundishia ili kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa wanafunzi na
jamii kwa ujumla.
Na leo tunaendelea kuboresha shule yetu ya Kiromo kwa
kutoa msaada wa uniform na viatu kwa wanafunzi. msaada wa sare za shule
tunazoto ni pamoja na Kaptura 600 , skirt 600 , mashati 1193 na viatu
728 vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 kwa shule ya msingi Kiromo.
"
Airtel Tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango
cha elimu hapa nchini na kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka na
upatikanaji wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. leo
tunathibitisha dhamira yetu ya kusaidia mashule kwa kutoa sare za shule
na viatu Kiromo shule ya msingi”, alisema Bayumi.
Airtel
itaendelea kusaidia mashule kwa kutoa vitabu na vifaa mbali mbali vya
kufundishia ikiwa ni sehemu ya shughuli zetu za kusaidia jamii, nia yetu
ni kuwafikia shule nyingi zaidi katika mikoa yote ya Tanzania
aliongeza. Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika
kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.
Tangu tulipoanza mradi wa “ shule
yetu” mpango wa kusaidia vitabu na vifaa vya shule , shule mbalimbali
nchini zimeshafaidika na mradi huu mpaka sasa.

.jpg)
No comments:
Post a Comment