Askari ambae hakuwa kwenye vazi rasmi akimsulubu mmoja wa wanafunzi mbele ya kituo cha polisi baada ya kukataa amri ya kuchuchumaa na kutembea kwa magoti hadi kituoni hapo. |
Mwanafunzi aliyeshikwa akipandishwa kwenye Difenda. |
Kundi hili lilijificha kwenye baa ya CCM iliyopo eneo hilo wakpigwa mabomu na kuchomolewa. |
Utakwenda Tu! |
Hiki ndicho kikosi Kizima kilicho dhibiti wanafunzi hao ndani ya dakika 15 tu! na wakanyooka. |
BAADA
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda
wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao
hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa,
waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka
mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi
wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa
maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo
ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa
na kuumia wengine walipoteza fahamu. Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa
na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya
utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova
aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya
tarehe 30 mwezi huu.
HAKI YA KULINDWA NI MUHIMU SANA IKAZINGATIWA OTHERWISE TUTAENDELEA KUSHUDIA WATANZANIA WANATESEKA NA KUFA KILA MARA KWA MABO YANAYOZUILIKA. POLISI WALINDE RAIA SIYO KUANZISHA FUJO
ReplyDelete