Tunajiunga na mfuko! Baada ya kueleweshwa faida za kujiunga na mfuko huo walikusanyika kwa mwandishi na kuanza kujiunga. |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo leo. |
Awali Mbunge huyo wa Mkuranga akisalimia viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga pamoja na wa Mfuko wa Afya ya jamii. |
Mbunge wa Mkuranga Mh.Adam Malima, akimkabidhi kadi ya uwanachama wa mfuko wa afya ya jamii Mzee Saleh Salum Kihedu mara baada ya kujiunga rasmi. |
WAKAZI
wa Kijiji cha Kimanzichana Wilayani Mkuranga Mkoani
Pwani wamejitokeza kwa wingi kujiunga kwenye mfuko wa afya ya jamii wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko huo unaosimamiwa na taasisi ya NHIF uliofanyika leo.
Timu ya kampeni ya uhamasishaji wa kujiunga
na mfuko huo ikiongozwa na mratibu wa CHF Rehani Athumani, itakuwepo wilayani
humo kwa kufanya uhamasishaji huo kwa njia mbalimbali zikiwemo za sinema na
mikutano ya hadhara, hadi mtandao huu unaondoka eneo la tukio zoezi hilo
lilikuwa likiendelea kwenye Kijiji hicho.
Mfuko wa afya ya jamii unaziwezesha kaya
husika kwenye halmashauri kupata matibabu kwenye hospitali za serikali kwenye
Wilaya husika kwa gharama ya Shilingi elfu tano kwa mwaka mzima huku kiwango
cha ukubwa wa familia ni Mkuu wa kaya na watoto watano wasiozidi umri wa miaka
18.
Wananchi wengi kwenye jimbo hilo
hawajajiunga kwenye mfuko huo, kutokana na taarifa iliyosomwa kwenye mkutano ni
kaya miasaba ( 700) tu kati ya kaya Hamsini na moja elfu (51,000) zilizopo
kwenye jimbo hilo.
Aidha kwenye uzindduzi huo ambao mgeni
rasmi alikuwa Mbunge wa jimbo la Mkuranga Kigoma Malima wananchi waliuliza
maswali mbalimbali kwa mbunge wao huku wakiwa na maswali mengi yaliyokuwa nnje
ya malengo ya mkutano huo ambayo hata hivyo mbunge huyo aliruhusu yaulizwe.
Akijibu baadhi ya maswali mbunge huyo
aliwataka wananchi hao kutopuuza fursa hizo ambazo ni za msingi huku
wakizingatia zaidi kwamba umuhimu huo upo zaidi kwa watoto na kina mama kwani
ndio huteseka zaidi kwenye suala la huduma za afya.
No comments:
Post a Comment