Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
Head
of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia
ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya
Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza
kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na
kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka
kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose
Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib,
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis
Nazrani.
Mkurugenzi
Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege
(wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba
wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa
vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na
watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo
usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.
Aidha
amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa
kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni
kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga
katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya kisasa.
Pichani Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Medics, Hospitali ya Aga Khan na waandishi wa habari walioshuhudia tukio la makabidhiano hayo.
Baadhi ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa rasmi leo kwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar ikiwa ni sehemu ya mradi Endelevu utakaohusisha Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa ajili ya kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto.
No comments:
Post a Comment