Ile staili ya kupakizana kwenye pikipiki watu watatu maarufu kama Mshikaki,ilimpelekea dogo huyu (mwenye fulana ya mistari) kutembezewa kichapo toka kwa Maaskari Polisi waliokuwepo kwenye moja ya kibanda cha Polisi wa usalama Barabarani kilichopo pembeni ya Barabara ya Uhuru na Kawawa pembeni mwa mataa ya kuongozea Magari pale Ilala Karume.Dogo huyu alifikia kuambulia kichapo hicho mara baada ya Askari mmoja alikuwa amevalia kiraia (kulia) kumtaka mwendesha pikipiki hiyo kusimama ambapo alitii amri hiyo na aliweza kusimama na kuwashusha wote waliokuwa wamepakiwa kwenye piki piki hiyo akiwemo Dogo huyu ambaye mkononi alikuwa ameshika bisibisi (ambayo haikufahamika alikuwa ametoka kuifanyia kazi gani wakati huo) na hapo ndipo lilipoanza balaa baada ya Askari huyo kuanza kumwambia kwanini ameshuka na bisibisi na kwamba alitaka kumchoma.Dogo huyo alikuwa akikana muda wote kuwa hakushika bisibisi hiyo kwa ubaya kwani alikuwa nayo toka huko walikotoka na baba yake (ambaye ndie alikuwa akiendesha pikipiki hiyo),mpaka Ripota wetu anaondoka eneo la tukio ilikuwa Dogo huyo yupo chini ya Ulinzi wa Polisi na hatujui kilichoendelea.Hiyo imekaaje wadau??
Saturday, January 12, 2013

Home
Unlabelled
Mshikaki wamsababishia dogo kupewa kichapo
Mshikaki wamsababishia dogo kupewa kichapo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment