Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Jospeh Warioba (kulia) akiongea na Mawaziri leo katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam katika mkutano uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yaokuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Nyamrunda akiongea
katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu
uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiongea katika mkutano
kati ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo
ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam
leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali (Mstaafu) Joseph Simbakalia akiongea katika
mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo kati
ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa
uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Wengine kutoka kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abass Kandoro, Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma)
na Bi. Chiku Galawa (Tanga).
Baadhi
ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatilia mkutano kati yao na
Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Makatibu Wakuu
na Manaibu Makatibu Wakuu kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Mawaziri Steven Wassira, Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika na Prof. Sospeter Muhongo wakifuatilia mkutano kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa nchini wakipata maelezo kuhusu mfumo wa uhifadhi wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya yanayowasilshwa katika Tume kwa maandishi kutoka kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bi. Flora Mkonya leo (Jumanne, Jan 15, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Kanali (Mstaafu) Joseph Simbakalia(Mtwara), Bw. Abass Kandoro (Mbeya), Bi. Chiku Galawa (Tanga).na Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma).Wakuu hao wa mikoa pia waliwaslisha maoni ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Katiba Mpya.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Al-Shymaa Kway-Geer, Bw. Humphrey Polepole na Bi. Riziki Mngwali wakifuatilia mkutano kati ya Tume na Mawaziri uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment