HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 19, 2013

KAMATI YA BUNGE YA ULINZI NA USALAMA YAFANYA ZIARA KATIKA GEREZA LA MAHABUSU LA SEGEREA, JIJINI DAR

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi, Mwamini Malemi akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu pamoja na kamati yake katika Gereza la Mahabusu la Segerea, jijini Dar es Salaam jana.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu pamoja na wajumbe wa kamati yake wakiwauliza maswali mbalimbali Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Segerea lililopo jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala Wafungwa na Mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi katika gereza hilo jana. Kamati hiyo ilitembelea sehemu wanapolala wafungwa na mahabusu, jikoni, ghala la chakula pamoja na kuzungumza na Maafisa wa Jeshi hilo na baadaye Mahabusu na Wafungwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali za Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) walipozitoa kupitia hotuba yao iliyotolewa wakati Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ziara katika gereza hilo jana.
 Afisa wa Magereza wa Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam, Gibson Mwakibibi akiwaonyesha mfuniko wa Hotpot (Chombo cha kuhifadhia chakula) pamoja na Radio Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ambapo vifaa hivyo vinatumika kuficha simu, visu, bangi na vifaa mbalimbali ambavyo ni hatari kwa usalama wa Mahabusu na wafungwa. Vifaa hivyo vilikuwa vinaingizwa na mahabusu hao pmaoja na baadhi ya ndugu zao wanapopeleka chakula gerezani hapo. Hata hivyo, maafisa magereza kwa kutumia chombo cha kugundulia vifaa mbalimbali (Metal Detector) kinachotumika gerezani hapo huvikamata vifaa hivyo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, John Chiligati akizungumza na maofisa wa Jeshi la Magereza wakati kamati hiyo ilipofanya ziara katika Gereza la Mahabusu la Segerea, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi. Kushoto ni  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad