HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 20, 2013

AJALI YA BASI LA NGANGA MMOJA AFARIKI PAPO HAPO NA MAJERUHI ZAIDI YA 40 WAPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

BASI LA KAMPUNI YA NGANGA LILILOKUWA LINATOKEA MBEYA KWENDA DAR ES SALAAM LIMEPINDUKA LEO KATIKA ENEO LA IMEZU NJE KIDOGO YA MJI WA MBEYA. AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MBILI ASUBUHI NA ABIRIA MMOJA  ALIFARIKI PAPO HAPO NA WENGINE ZAIDI YA 40 WAMEJERUHIWA VIBAYA NA KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MJINI MBEYA. ABIRIA ALIYEFARIKI AMETAMBUWA KWA JINA LA ENOCK LWILA MKAZI WA ENEO LA MAMA JOHN MJINI MBEYA NA NIMFANYABIASHARA KWENYE SOKO LA MWANJELWA
BAADHI YA WAKAZI WA IMEZU WAMESEMA AJALI HIYO IMESABABISHWA NA MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI HILO.


MWILI WA MAREHEMU ENOCK LWILA  UKIWA UMELAZWA CHINI KUSUBIRI WANA USALAMA KUJA KUUCHUKUA.MAREHEMU ENOCK LWILA AMEKUTWA NA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 KATIKA SOKSI NA KWENYE MIFUKO YAKE YA SURUALI INASEMEKEANA ALIKUWA ANAENDA DAR ES SALAAM KUNUNUA BIDHAA MBALIMBALI ZA DUKANI KWAKE.


HAPA WANAUSALAMA WAKIHESABU PESA WALIZOZIKUTA KWENYE MWILI WA MAREHEMU ENOCK HUKU WANANCHI WAKISIMAMIA KWA MAKINI ZOEZI HILO LA KUHESABU HIZO PESA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15  ALIZOKUWANAZO MAREHEMU 

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG.

1 comment:

Post Bottom Ad