HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 27, 2012

WATANZANIA MBWANA MATUMLA NA MADA MAUGO WATOA VICHAPO KWA WAPINZANI WAO

Bondia Mada Maugo (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumtwanga bondia Yiga Juma (Uganda) kwa ‘Knock Out’ raundi ya kwanza.
Bondia Mbwana Matumla (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumpa kichapo bondia David Charanga (Kenya).
Mada Maugo (kushoto) akimshushia kichapo bondia Yiga Juma (Uganda) wakati wa mpambano wao.
Bondia Mbwana Matumla (kulia) akitupiana makonde na bondia David Charanga kutoka Kenya.
Bondia David Charanga kutoka Kenya (kulia) akienda chini baada ya kupokea konde kutoka kwa Mbwana Matumla.
David Charanga kutoka Kenya (kulia) akimkabili bondia Mbwana Matumla wakati wa mpambano wao jana.
--
Mabondia wa Tanzania jana waling'ara katika mapambano yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem. Bondia maarufu nchini, Mada Maugo alimchapa Yiga Juma kutoka Uganda raundi ya kwanza kwa ‘Knock Out’. Katika hali iliyoonesha kuwa siku ya vichapo kwa wageni, pambano lingine ambalo bondia Mbwana Matumla alipambana na bondia kutoka Kenya, David Charanga lililokuwa la raundi nane, Matumla aliibuka kidedea katika raundi zote nane na kumfanya aibuke na ushindi wa kishindo.
(PICHA NA ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad