HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2012

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KATA YA KIPAWA WAPATA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA UJASIRIAMALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Dk. Makongoro Mahanga (aliesimama) akizungumza wakati alipokuwa akifungua Mafunzo ya Ufundi Stadi na Ujasiriamali kwa Wanawake wa Kata ya Kipawa yaliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Air Wing,Ukonga jijini Dar.Kulia ni Diwani wa Kata hiyo ya Kipawa na Mratibu wa Mafunzo hayo,Bonnah Kaluwa na kushoto ni Msaidizi wa Naibu Waziri,Bw. Mohamed na wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo,Said Fundi.
Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Dk. Makongoro Mahanga kufungua mafunzo ya Wanawake Wajasiriamali wa Kata ya Kipawa.
Mgeni rasmi Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto), Msaidizi wa Waziri,Bw. Mohamed, Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said Fundi (wa pili kushoto), Diwani wa Kata ya Kipawa, Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Lucy Semendu (kulia) na Mwakilishi kutoka Kampuni ya Darling ambao ni wadhamini wa mafunzo hayo wakipiga makofi kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mafunzo hayo.
Wakina mama wajasiriamali wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala wakishangilia wakati semina yao ya siku moja ya mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake iliyofanyika ukumbi wa Air Wing Dar es Salaam ikiendelea. Semina hiyo ilifadhiliwa na Benki ya Equity na Darling Hair kwa msaada wa Diwani wa Kata hiyo Bonnah Kaluwa.
wanawake hao Wajasiriamali wakijiandikisha kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Wakina mama hao wakiwa katika mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad