Duka la Mavazi ya Kisasa na yenye hadhi ya Kimataifa la J&M Virgo linasherehekea Mwaka mmoja toka kuanza kwake,huku likitoa shukrani nyingi kwa wateja wake na wadau mbali mbali,ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa ni sehemu ya mafanikiwa kwa Duka hili kufikia hapo walipo sasa.Pamoja na kusherehekea kwao Mwaka mmoja tangu kufunguliwa kwa Duka hilo,pia wameleta mali mpya kibao toka USA,Italy,UK na Turkey kwa ajili ya msimu wa Sikukuu za Krismass na Mwaka Mpya.
Wakurugenzi wa Duka la Mavazi la J&M Virgo,James na Mishy wakikata keki iliyoandaliwa kwa ajili ya hafla fupi ya kusherehekea Mwaka mmoja wa Duka lao hilo toka lianzishe,iliyofanyika Dukani kwao hapo,Mikocheni kwa Warioba,jijini Dar ndani ya jengo jipya la C&G Plaza.Pamoja na kusherehekea kwao Mwaka mmoja tangu kufunguliwa kwa Duka hilo,pia wameleta mali mpya kibao toka Ughaibuni kwa ajili ya msimu wa Sikukuu za Krismass na Mwaka Mpya.
Wakurugenzi wa Duka la J&M Virgo,Da' Mishy (kulia) na Mdau James (pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na timu yao nzima,huku wakiwa wamepigilia pamba za nguvu ambazo ni sehemu ya mzigo mpya ulioingia hivi karibuni Dukani hapo,Mikocheni kwa Warioba,jijini Dar ndani ya jengo jipya la C&G Plaza,ambapo sasa wapo na ofa ya msimu wa Krismas na Mwaka mpya.Fika dukani kwao hapo na ujipatia vitu vya ukweli.
Magauni makali kwa kina dada.
Moka za ngunu kwa kina Baba.
Michuchumio ya uhakika kwa kina Dada.
No comments:
Post a Comment