Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Marison Mwakyoma akiongea na madereva wa Boda Boda kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa wazi uliopo kata ya kimandolu jijini Arusha.(Picha na Mahmoud Ahmad - Arusha)
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Mkuu huyo wa Usalama barabarani amesema ameanzisha kampeni hiyo ili kila mmoja apate mafunzo yake kupitia chuo hali ambayo itasaidia kupunguza ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa.
Mkutano huo uliohudhuriwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi Gilles Muroto, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi toka Dawati la Jinsia na Watoto, Maria Maswa, Polisi tarafa, viongozi wa tarafa ya Suye, kata, mitaa na madereva wapatao 100 ulitawaliwa na makofi ya pongezi pamoja na vifijo kutoka kwa madeva hao baada ya Mkuu huyo wa Usalama Barabarani kuwaahidi kuwa kama wangekuwa tayari hata siku ya pili yake (jana) wangeweza kuanza darasa.
Alimalizia kwa kuwaasa madereva hao kutojichukulia sheria mkononi pindi mwenzao anapogongwa na gari kwani vitendo hivyo vinaweza kuwagharimu badala yake aliwataka wafanye mambo manne muhimu; kwanza kuandika namba ya gari iliyosababisha ajali, kuielewa mahali ajali ilipotokea, kutoa taarifa polisi na mwisho kumwahisha mwenzao hospitali.
Programu ya mafunzo kwa waendesha pikipiki mkoani hapa ilianza rasmi mwezi Agosti mwaka huu baada ya kufunguliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la ajali.
Hadi sasa waendesha boda boda wapatao 900 kutoka wilaya za Arusha mjini, Arumeru na Monduli wamekwisha pata mafunzo ya udereva toka vyuo mbalimbali vilivyopo mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment