Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiangalia kahawa katika shamba darasa inayolimwa na Ibrahim Mulokozi (kulia) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba aliyenufaika na mkopo wa shilingi laki nne kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea shamba hilo la kahawa na migomba jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kutoka SACCOS ya Ibwera zimewanufaishaje kimaisha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
akiangalia shamba darasa la kahawa na migomba la mkazi wa kijiji cha
Ibwera wilayani Bukoba Ibrahim Mulokozi (hayupo pichani) wakati
alipolitembelea jana ili kuona fedha za mkopo wa mfuko wa vijana
alizozipata kupitia SACCOS ya Ibwera zimemnufaishaje kimaisha. Kushoto
ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimuangalia samaki mwenye umri wa miezi mitatu anayefugwa katika bwawa la Kikundi cha Msifuni kilichopo kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea bwawa hilo jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kupitia mfuko wa Halmashauri nimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa tatu
kulia) akiangalia jana nyavu za kuvulia samaki za Kikundi cha Msifuni
kilichopo katika kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata
mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuanzisha mradi wa bwawa la
samaki. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Johanes Joel.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo wilayani Bukoba kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS hiyo ilipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa SACCOS ya Ibwera na viongozi wa wilaya ya Bukoba wakati alipowatembelea jana ili kuona fedha walizopata kutoka mfuko wa waendeleo ya vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment