HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 29, 2012

kumbukumbu ya mtangazaji halima mchuka

Leo Jumamosi Dec 29 ni mwaka mmoja tokea mtangazaji wa kwanza wa kike kutangaza mpira katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati Halima Mchuka (pichani) kufariki dunia.

Halima Mchuka atakumbukwa kwa weledi wake wa hali ya juu katika tasnia ya utangazaji, hasa wa mpira ambapo aliweza kubuni maneno na majina mengi ambayo yanatumika hadi hii leo, mfano mkubwa ni 'mpira umeenda fyongo' akimaanisha mpira umepigwa vibaya na mchezaji.

Leo saa kumi jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa dada yake  Mwajuma Mchuka Mbezi Beach, Dar es salaam. Karibuni wote kumuenzi na kumuombea dua  shujaa huyu.

1 comment:

  1. Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani.. She was one of a kind lady.. Very very hardworking and never complains.. Haitatokea tena someone like her..

    ReplyDelete

Post Bottom Ad