Kwanza
kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Muumba wa
Mbingu na Ardhi kwa kuweza kutufanikisha kufika siku ya leo tukiwa hai na wazima wa afya,kwani kuna wenzetu wengine hawakuweza kabisa fika siku ya kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu.hivyo ni jambo la kumshukuru sana Muumba kwa kutujaalia kufika siku ya
leo.
Pia napenda kutoa Shukrani zilizo za Dhati kabisa kwa wadau woote na wapenzi wa libeneke letu hili la Mtaa kwa Mtaa Blog kwani bila nyie,wala kusinge kuwa na libeneke hili ambalo kiukweli ni libeneke linalopendwa na wengi,hasa kutokana na muendelezo wa matukio yake.Nawashukuru sana Wadau wa Mtaa kwa Mtaa Blog.
Shukrani zingine ziwafikie wadhamini wetu wa Blogu yetu hii,ammbao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakitoa mchango mkubwa sana katika muendelezo wa Libeneke letu hili.Shukrani sana kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF),Hoteli ya Hill View ya jijini Mbeya pamoja na Shule ya Awali ya Dream.Shukrani sana kwenu.
Kwa heshima na taadhima napenda pia kutoa shukrani za dhati kwa Wanalibeke wenzangu woote waliopo ndani na nje ya nchini chini ya uongozi wake mkongwe Muhidin Issa Michuzi a.k.a Ankal a.k.a mzee wa Fulanazz,mzee wa Libeneke na majina mengine mengi aliyonayo,kwani kiukweli yeye ndie ametufungua macho wanalibeneke wengi wa ndani na nje ya nchini.Shukrani sana na za kipekee kwa Ankal Michuzi ambaye ni mmiliki kiongozi wa Libeneke la Globu ya Jamii.
hivyo wote wa pamoja napenda kuwatakia kila lililo la kheri katika kuanza kwa Mwaka mpya wa 2013.
Nasema Ahsanteni sana na Tuko PamoJah.
YAANI NIKWELI KABISA,HATA MIMI NAMSHUKURU MUNGU SANA TU PAKA HAPA NILIPOFIKIA NA KUUONA MWAKA MPYA,UNAWEZA KUTEMBELEA BLOG ZANGU,ASALAAM ALEYKUM.....................
ReplyDelete