HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 7, 2012

Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi ya SADC jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya nchi za Jumuiya uchumi na maendeleo ya Kusini (SADC) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini ili kushiriki kikao cha kamati hiyo.Pembeni ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete( Wanne Kushoto) akiwa na viongozi SADC waliopo katika kamati hiyo.Wengine katika picha ni Rais Wa Afrika ya Kusini Jackob Zuma(Watatu kushoto), Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(kulia),Rais Mstaafu wa Msumbiji ambaye pia ni msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Madagaska, Joachim Chissano(wapili kushoto) na kushoto ni Katibu mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini(kulia) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Msumbiji ambaye pia ni msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Madagaska, Joachim Chissano,Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini( wa pili kulia).Picha na Freddy Maro,Ikulu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad