
Shughuli kubwa iliyofanywa na mtoto mdogo Gozbert Bwere (3)katika upigaji wa ngoma ndiyo iliyowafanya baadhi ya viongozi wa kisiasa na Serikali kuenda kumtunza mtoto huyo, ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM Nape Nnauye na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mwigulu Nchemba walienda na kumtunza mtoto huyo kwa umahiri wake katika kupiga ngoma.
Jana nilipita maeneo ya Manzese katika moja ya kiota cha siku nyingi Frieds Coner na kumkuta mmoja wa wanakikundi akiwa na watoto hao nje ya hoteli hiyo,akajitambulisha kwamba yeye ni Mpalala Mwendwa na ni msaidizi wa Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara akaongeza na kusema yeye amefuatana na kikundi hicho kama mmoja wa viongozi wa msafara kutoka mkoani Mara.
Kilichinisikitisha sana ni kiongozi huyo kuonekana akiwa ameshika chupa ya pombe kali aina ya Value akionekana kuwanywesha watoto hao pombe hiyo kwa kifuniko cha chupa hiyo, huku mtoto Gozbert Bwere akikunja sura mara baada ya kunywa pombe hiyo ikiwa ni kuashiria kwamba hawezi kumudu kuinywa.
Kitu kilichiniumiza sana nilipoongea na Bwana Mpalala Mwendwa aliniamba kuwa wazazi wa watoto hao wamebaki Musoma.
Hivyo watoto hao wako chini ya uangalizi wa kikundi hicho pekee jambo ambalo si jema na kuna uwezekano mkubwa wa kumomonyoka kwa maadili ya watoto hao, kwani hawana ulinzi wa kotosha kama ilivyoshuhudiwa jana wakiwa wananyweshwa pombe hiyo ya Value na kiongozi huyo.
(NA FULLSHANGWEBLOG.COM)

No comments:
Post a Comment