Mwakilishi wa Mfuko wa bima ya Afya (NHIF) mkoani Lindi Bi, Fortunata Raymond wa tatu kutoka kulia pamoja na wafanyakazi wenzake, wakionyesha cheti walichokabidhiwa na kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Mjini Lindi jana, kutokana na ushiriki wao kwenye maadhimisho hayo.
Kazi kubwa iliyofanywa na maafisa wa (NHIF) ilikuwa kuelimisha wananchi na kuwapa maelezo wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na mifuko ya afya ya jamii ili kuboresha afya zao pamoja na familia zao.
Mwakilishi wa NHIF mkoani Lindi Bi. Fortunata Raymond wa tatu kutoka kulia akiongoza wafanyakazi wa mfuko huo kupita mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwa maandamano wakiingia kwenye uwanja wa Ilulu kwa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika jana mjini Lindi.
Wasanii wa vichekesho wanaojulukana kama Shoti na Hasara wakiaga mashabiki wao mara baada ya kuwavunja mbavu wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi jana.
No comments:
Post a Comment