Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania usharika wa Msasani jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa DVD ya Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi la kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa ambaye aliongozana na familia yake yote, alichangia shilingi millioni 10, huku wanawe wakitoa kiasi cha shilingi milioni tano.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akipongezwa na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania usharika wa Msasani,Eliguard Muro mara baada ya kuhutubia na kuzingua DVD ya kwaya ya Kanisa hilo na kuendesha Harambee ya Kuchanfia Ununuzi wa Basi la Kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB,Dk. Charles Kimei (kulia) akiwahamasisha waumini wengine kujitokeza kuchangia Harambee hiyo,ambapo yeye binafsi aliweza kuchangia kiasi cha Sh. Milioni 7 katika harambee hiyo.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ambaye ndie alieiongoza harambee hiyo.
Mdau Richard Kasesela akichangia kiasi cha Dola 300 katika harambee hiyo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa DVD ya Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi la kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mke Waziri Mkuu Mstaafu,Mkewe Mama Regina Lowassa (kushoto) akiwa na Familia yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa DVD ya Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi la kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment