HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 19, 2012

Neno La Leo kutoka kwa Mjengwa: Kitendawili Cha Embe Dodo Na Tunakokwenda...

Ndugu zangu,

Jana alasiri pale Bagamoyo nilisimama kununua embe dodo. Akina mama wale wakarimu walinipokea kama mwenzao. Bei ya dodo niliyotajiwa ilinifanya pia nitafakari sana, niingiwe na huzuni pia. 

Maana, ni ukweli, kuwa mama yule anaanza kuzitafuta dodo zinakotoka, kisha anazipanga pale chini mchangani. Bei ya dodo kubwa kabisa ni shilingi mia sita! 

Nilinunua dodo saba. Na hesabu ya dodo saba ikampa tabu sana mama yule. Akaniomba nimsaidie hesabu ya haraka. Nikamwambia ni shilingi 4,200. Kwenye noti ya elfu tano niliyompa alihitaji kunirudishia shilingi mia nane. Nikamwambia aitunze chenji hiyo. 

Akashukuru , lakini, wakati akinifungia dodo zangu akaniongeza dodo mbili! Hivyo, kimsingi ameniongeza dodo za thamnani ya 1200! Hivyo, ile mia nane niliyomwachia haina faida kwake. Unafanyaje?

Njiani niliwaza juu ya tunakokwenda kama nchi.Tujiulize; hivi rasilimali zetu za nchi ikiwamo madini, gesi na mafuta tunayoambiwa tunayo kwa wingi yatamsaidia vipi mama yule wa Bagamoyo mwuza embe dodo ambaye yumkini hajui kusoma, kuandika na kuhesabu? 

Na idadi yao inazidi kuongezeka. Takwimu zinasema; asilimia 39 ya Watanzania milioni 45 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu. Na hawa wanawaririthisha nini watoto wao?

Kila kizazi na Jukumu Lake; Tafakari,Chukua Jukumu La Kizazi Chako.... Na hilo Ni Neno La Leo. 

Maggid Mjengwa,

2 comments:

  1. Hili neno la 'Tafakari...Chukua Hatua' nalo ni siasa tupu...Hebu nieleze mimi nichukue hatua gani nzuri unayoifikiria, kunambia tu nitafakari na kuchukua hatua, tayari kutafakari pekee ni kuchukua hatua...hebu tusiingie kwenye mikumbo ya kisiasa..

    ReplyDelete
  2. ".... RULAR DEVELOPMENT IS THE PARTICIPATION OF PEOPLE
    IN A MUTUAL LEARNING EXPERIENCE INVOLVING THEMSELVES,
    THEIR LOCAL RESOURCES, EXTERNAL CHANGE AGENTS,AND OUTSIDE RESOURCES.
    PEOPLE CAN NOT BE DEVELOPED, THEY CAN ONLY DEVELOP THEMSELVES BY
    PARTICIPATING IN ACTIVITIES WHICH AFFECT THEIR WELL-BEING
    PEOPLE ARE NOT BEING DEVELOPED WHEN THEY ARE HERDED LIKE ANIMALS INTO NEW VENTURES….J.K.NYERERE 1968

    ReplyDelete

Post Bottom Ad