HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 19, 2012

MAMA SALMA KIKWETE KUZINDUA HUDUMA ZA NHIF KESHO

MFUKO wa Taifa wa Taifa wa Afya (NHIF) kesho unazindua rasmi mpango wa huduma za bima ya afya kwa vikundi vya wajasiriamali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete.

Uzinduzi huo utafungua milango kwa vikundi mbalimbali kujiunga na huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo wafanyakazi wa Sekta rasmi tu ndio walipewa nafasi ya kutumia huduma hizo.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, inasema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 2.30 asubuhi.

Taarifa hiyo imesema kwamba uzinduzi wa mpango huo unatoa fursa kubwa kwa Watanzania kuhakikisha wanaingia kwenye utaratibu wa bima ya afya ili wawe na uhakika wa kupata matibabu.

“Hii ni fursa nyingine ambayo Mfuko imeona iitoe kwa Watanzania na hii inatokana na ukweli kwamba huduma za matibabu zimekuwa zikipanda kila kukicha na wananchi wengi kushindwa kumudu gharama hizo na wakati mwingine kusababisha madhara makubwa yakiwemo ya kupoteza maisha…mtu akiwa kwenye utaratibu wa bima anakuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wowote hata kama hana fedha mfukoni,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Shughuli kubwa zitakazofanyika katika uzinduzi huo ni pamoja na kuzindua huduma hiyo, kugawa vitambulisho vya matibabu kwa wanachama wapya ambao wamejiunga kupitia vikundi vya wajasiriamali vinavyoratibiwa na WAMA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad