HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 18, 2012

Mshindi wa tatu Epiq BSS-Wababa Mtuka kuachia wimbo wake mpya kesho

Yule mkali ambaye wengi walitarajia kuwa angeibuka na kitita cha shilingi milioni 50, Wababa Mtuka, anatarajia kuaachia singo yake mpya ya kwanza itakayojulikana kwa jina la  ‘MY WIFE’ ,ambayo ameirekodia Surround Sound Studios chini ya mtayarishaji  EMA the Boy.

Wababa, ambaye alitoa ushindani mkali kwa Walter na Salma, amesema anaamini wimbo huo utakuwa mkali na utashika sana wapenda burudani hapa nchini. ‘Nimetoa wimbo huu kama zawadi ya sikukuu kwa mashabiki wangu wote ambao wamenisapoti kipindi chote cha mashindano, lakini pia shukrani za pekee ziende kwa Zantel kwa kunirekodia wimbo huu’ alisema Wababa.

Wimbo huo, ambao ndio wa kwanza kutambulishwa kati ya nyimbo zote za washiriki wa Epiq BSS, umedhaminiwa na kampuni ya Zantel kama ahadi yake ya kuwarekodia bure wasanii waliongia 12 bora ya Epiq BSS. Nyimbo nyingine za washiriki wa Epiq BSS zitaachiwa mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad