Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na
viongozi wa Wilaya mpya ya Kalambo alipotembelea hivi karibuni kuona jengo
ambalo Mkuu wa Wilaya hiyo atalitumia kama ofisi yake ya muda.
Aliwataka viongozi pamoja na watumishi kutoweka urasimu mbele katika
utendaji kazi na badala yake kuwa kitu kimoja bila kujali cheo cha mtu.
"Kila mmoja atekeleze jukumu lake katika eneo lake na kwa kufanya hivyo
kutaifanya Wilaya hii nzuri kusonga mbele kwa kasi, kwa watumishi wa kada
za chini mnatakiwa kumuona Mkuu wa Wilaya kama rafiki na kumuona muda
wowote pale ushauri wake unapohitajika" alisema Injinia
Manyanya.
Kushoto na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Kalambo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
alipotembelea kuona hali ya ofisi hiyo, Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo
machachari ndugu Moshi Mussa Chang'a. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka viongozi
hao kuhakikisha suala la mipango miji bora linazingatiwa katika kupanga
miji na wilaya kwa ujumla.
Mazungumzo yakiendelea, hata hivo Mkuu huyo wa Mkoa aliwaomba
viongozi hao kuwa wavumilivu kwani kutokana na
changamoto.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akielezea baadhi
ya kero zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Mkuu huyo
wa Mkoa aliwapa moyo kuwa watumie uwezo wao mdogo walionao kutatua baadhi
ya kero hizo na nyingine watashirikiana kuhakikisha zinapatiwa
ufumbuzi.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya na viongozi pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya mpya ya Kalambo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Moshi
Chang'a.
Jengo ambalo linatumika kwa muda kama Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
ya Kalambo.
Makazi ya muda ya Mkuu wa Wilaya hiyo.(Na Hamza Temba - rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment