Askofu Msaidi wa Jimbo Kuu la
Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa (katikati) akiongoza ibada ya
mkesha wa Sikuu ya Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini
Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Paroko wa kanisa hilo, Padri, Joseph Mosha. (Picha na Habari Mseto Blog)
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Krismasi leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa baraka kwa waumini wa Usharika wa Azania Front baada ya ibada ya Krismasi
Mmiliki wa Mtandao wa Kijamii wa Kimbunga Net, Dotto Mwaibale akipeana mkono na Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Alex Malasusa baada ya ibada ya Krismasi iliyofanyika leo katika Usharika wa Azania Front. Kulia ni mmiliki wa mtandao wa Mzuka wa Fungo, Omary Fungo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiwa amembeba mtoto, Prisca John Mkony. Kushoto ni Sia Robinson na Jane Mkony akiwa amembeba mtoto, Patricia.
Baadhi ya
waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph wakiwa katika ibada ya Sikukuu ya Krismas.
Mkurugenzi wa Free Media Ltd, Liliani Mtei (kulia) akiwa na baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) wakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Askofu
wa kanisa hilo, Dk Alex Malasusa (hayupo pichani) wakati wa ibada ya Krismasi
iliyofanyika.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akipeana mkono na muumini wa kanisa hilo,
Sevestine Mtunga baada ya ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika
kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya akinamama waliojifungua wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Krismasi wakiwa na
watoto wao katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana. Kutoka
kushoto ni Fatuma Shaban mkazi wa
Vingunguti, Lucy Dominick mkazi wa Mwananyamala na Moshi Mengi mkazi wa Manzese
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akitoa Baraka kwa mtoto, Patricia John Mkony mara baada ya ibada ya Sikukuu ya Krisimasi iliyofanyika katika kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Rubani Mkuu mstaafu wa Serikali, Kapteni John Mkony, Jane John na Sia Robinson.
Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia mpya ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi wakifuatilia sehemu ya ibada ya Krisamsi iliyokuwa ikiendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, Dar es Salaam leo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Muadhama Polycarp Kadinali Pengo akipokea michango mbalimbali ya fedha kutoka kwa viongozi wa jumuiya za kikristo katika jimbo la segerea, dar es salaam alipokwenda kuongoza ibada ya Krismasi sambamba na uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Bonaventure, Kinyerezi, Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment