Mwanamuziki Koffi Charles Antwaa Olomide akijimwaya mwaya kwa madaha kabisa jukwaani kwenye Tamasha la Tusker Carnival,huku akishangiliwa na umati mkubwa watu uliohudhuria tamasha hilo,lililofanyika Usiku wa Kuamkia leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar.
Mwanamuziki
mahiri wa Bendi ya Quartie Latin aitwae Cindy, linaloongozwa na nyota
wa muziki wa dansi kutoka nchini DRC-Congo,Koffi Olomide akiimba
jukwaani mbele ya umati mkubwa wa watanzania uliojitokeza kwenye Tamasha
la Tusker Carnival ndani ya viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini
Dar.
Pichani juu na chini ni Mwanamuziki wa Kimataifa Koffi Olomide sambamba na skwadi lake la Quartie Latin.
Mmoja wa Madansa wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Quartie Latin chini yake Mkongwe Mapao Koffi Charles Antwaa Olomide akionyesha umahiri wake wa kulishambulia jukwaa.
Mkali wa Muziki wa Dansi toka Nchini Congo DRC,Mapao Koffi Charles Antwaa Olomide akiyarudi magona na mmoja wa warembo wataoshiriki katika shindano la Miss East Afrika linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Dansa wa kike wa Quartie Latin akifanya mambo yake stejini.
Wanamwita Mapao Koffi Charles Antwaa Olomide akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa Tamasha la Tusker Carnival lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar usiku wa kuamkia leo.
Koffi Olomide akiwatambulisha waimbaji wake wa kike.
Madansa wa kike wa Bendi ya Quartie Latin chini yake Mkongwe Mapao Koffi Charles Antwaa Olomide akionyesha umahiri wake wa kulishambulia jukwaa.
Wanamuziki wa Bendi ya Skylight wakionyesha umahiri wao wa kulishambulia jukwaa kwenye Tamasha la Tusker Carnival kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Wanamuziki wa Bendi ya Diamond Musica wakifanya mambo yao jukwaani kwenye Tamasha la Tusker Carnival kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Madansa wa Bendi ya Twanga Pepeta wakiwachengua Mashabiki wao wakati wa muendelezo wa Tamasha la Tusker Carnival linaloendelea usiku huu kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Ephrahim Mafuru (katikati),Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Nandi Mwiyombela na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacoma Tanzania,Kelvin Twissa wakibadilishana mawazo wakati wa muendelezo wa Tamasha la Tusker Carnival kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijinin Dar es Salaam.
Wadau.
Shangwe kwa Mashabiki wa Muziki wa Dansi jijini Dar.
No comments:
Post a Comment