HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 4, 2012

Kampuni ya Jambo Concepts yazindua gazeti jipya la DarMetro jijini Dar leo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited,Juma Pinto akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Gazeti Jipya la Matangazo liitwalo DarMetro ambalo litakuwa linatolewa Bure kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam,iliyofanyika jioni hii katika kiota cha City Sports Lounge kilicopo katikati ya jiji la Dar.

Meneja Mkuu wa Jambo Concepts, Ramadhan Kibanike akizungumza machache muda mfupi kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa Gazeti Jipya la Matangazo liitwalo DarMetro ambalo litakuwa linatolewa Bure kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
 Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited,Juma Pinto,Meneja wa Matangazo wa DarMetro,Lightness Sirikwa pamoja na Mhariri Mkuu wa Gazeti hilo la DarMetro,Yakobe Chiwambo wakionyesha Muonekano wa Gazeti hilo wakati wa Uzinduzi wake uliofanyika jioni hii kwenye kiota cha City Sports Lounge,Jijini Dar.
 Baadhi ya wadau mbali mbali wa jijini Dar wakiwa kwenye hafla hiyo iliofanyika jioni hii kwenye kiota cha City Sports Lounge,Jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad