Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Azam.
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akiipangua ngome ya Azam kabla ya kuachia kiki kali na kuipatia timu yake bao la kwanza.hadi mwisho wa Mchezo Yanga 2-0 Azam.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kushoto) akichuana na beki wa Azam, FC, Said Morad katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia
Golikipa wa Azam, Ally Mwadini akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wao dhidi ya Yanga uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.Yanga imeshinda bao 2-0.Huko Morogoro nako leo Mnyama (timu ya Simba) avutwa sharubu mchana kweupeeee,baada ya kuchezea kichapo cha Bao 2-0 kutoka kwa Wakata Miwa wa Mkoa huo,timu ya Mtibwa Suger.kwa matokeo ya leo,Timu ya Yanga ndio inayoshika usukani wa Ligi kuu kwa kuwa na point 26.
Balozi wa FIFA, Abeid Pele (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa TFF pamoja na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto wakati alipohudhuria mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kati ya Yanga na Azam FC kwenye uliuofanyika leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pele yupo nchini kwa ajili ya programu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). (Picha zote na Habari Mseto Blog)
No comments:
Post a Comment