Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Washiriki wa Maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya Mabango yenye Ujumbe wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya Wawanake.
Maandanamo yakipokelewa na Muwakilishi wa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora Msechu (wa tatu kulia),Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema (pili kulia) pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Charles Kenyera.
Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan akikata utepe uliokuwepo kwenye basi aina ya Toyota Coster,ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Safari ya Wadau wa Wildaf wanaokwenda Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali katika mikoa ya kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya Wanawake.
Wadau wa Wildaf wakipanda kwenye Basi hilo tayari kwa Safari ya Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali katika mikoa ya Kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya Wanawake.
Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula (pili kupia) akitoa neno la Ukaribisho katika Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.Wengine Pichani toka kulia ni,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Mkurugenzi wa Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora Msechu,Mkugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Judith Odunga pamoja na Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan.
Muongozaji wa Mkutano huo,alikuwa ni Bw. Deus Kibamba
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini,DCP Rashid Omar akiwasilisha mada ya aina mpya ya Karatasi maalum itolewayo na Polisi iwapo mtu anapatwa na tatizo la Majeraha (PF 3) iliyofanyiwa Marekebisho na kuongezewa baadhi ya Vipengele Muhimu,wakati wa Mkutano uliofanyika leo wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya Wanawake,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akisoma Hotaba yake mbele ya Mamia ya Wadau wa Wildaf waliohudhulia Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akikata Utepe wa Kuashiria Uzinduzi rasmi wa aina mpya ya PF 3 mara baada ya kutoa Hotuba yake huku akisaidiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa Makini.
Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kipolisi ya Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema akiteta jambo na Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Mrisho Mpoti na Mjomba Band wakitoa Burudani wakati wa Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment