Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sherehe za Siku ya Familia ‘Familiy Day’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhusisha wafanyakazi wa benki hiyo na familia zao.
WATANZANIA
wametakiwa kupanua wigo wa maendeleo yao kiuchumi, ngazi ya mtu mmoja
mmoja, familia na taifa, kwa kujiunga na kutumia ipasavyo huduma ya
‘SimBanking’ inayotolewa na Benki ya CRDB
Hayo
yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk Charles
Kimei, wakati wa sherehe za kila mwaka za Siku ya Familia ‘Family Day’
inayohusisha wafanyakzi wa benki hiyo na familia zao, iliyofanyika
kwenye Hoteli ya Kunduchi Welt ‘n’ World’ jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa, kila mwaka wa sherehe hizo huwa na huduma moja inayotangazwa,
ambapo mwaka huu kipaumbele ni huduma ya ‘SimBanking’ iliyozinduliwa
Aprili, ikiwa na lengo la kurahisisha maisha ya wateja na kuwapa fursa
ya kuachana na ukiritimba wa kupata huduma za benki kwa kupoteza muda
mwingi kwenye foleni.
Aliongeza
kuwa, huduma hiyo ni ya kipekee miongoni mwa mabenki nchini, inayoweza
kuchangia upanuzi wa maendeleo ya kielimu, kiuchumi na kijamii, kwa
kumpa fursa mteja kuhamisha fedha kwenda akaunti yoyote ndani ya mtandao
wa CRDB.
“Huduma
hii inasaidia huhamisha fedha kwenda kwenye simu ya mkononi ya mtandao
wowote nchini, kulipia ankara (bili) mbalimbali, kununua muda wa
maongezi kwa mitandao yote chini, kununua umeme wa LUKU, kutuma na
kuchukua fedha kwenye ATM bila kadi ya benki hata kama aliyetumiwa hana
akaunti ya benki hiyo,” alisema.
Akizungumzia
sherehe hizo, Dk Kimei alisema kuwa ‘Family Day’ husaidia kuwaweka
pamoja wafanyakazi na familia zao, ili kuzungumza, kujifunza,
kubadilishana mawazo, kuimarisha ushirikiano miongoni mwao, jambo ambalo
haliwezi kufanyika kirahisi kutokana na mgawanyiko wa matawi na ofisi
zao.
Aidha,
aliongeza kuwa, kwa miezi 11 ya mwaka huu wameweza kuajiri zaidi ya
wafanyakazi 700 na kufanya orodha ya waajiriwa katika benki hiyo
kuongezeka zaidi, ambapo ujazo wa faida kwa mwaka ukiwa ni asilimia 15,
huku akitarajia ongezeko la asilimia hizo kwa Desemba.
“Wastani
wa miaka iliyotangulia ya ujazo wa faida ni asilimia 18 hadi 20 kwa
mwaka na kutokana na ukweli kuwa hii ni Novemba, tunatarajia ongezo hilo
kwa Desemba ili kufikia ama kuvuka kiwango cha miaka iliyopita,”
alisema.
No comments:
Post a Comment