HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 30, 2012

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za misiba ya wasanii watatu wa tasnia ya filamu na muziki nchini.

“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya vifo hivi vya wasanii hawa John Mganga, Mlopelo na Hussein Mkeity a.k.a Sharo Milionea ambao mchango wao unahitajika sana katika tasnia ya sanaa, pengo waliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wao bado unahitajika katika tasnia hii.”

Baraza linatoa pole kwa familia za marehemu na wasanii wote nchini, aidha linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na wapendwa wetu.

Tunaomba mwenyezi Mungu azipumzishe mahala pema peponi roho za marehemu. Baraza liko pamoja na familia za marehemu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tutambue kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.

Imetolewa na
Ghonche materego
Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad