Mkazi wa kisiwani Goziba akitumia simu ya kiganjani muda mfupi baada ya kampuni ya Vodacom kuzindua rasmi huduma zake kisiwani humo ikiwa ni kampuni ya kwanza kufikisha huduma za simu Kisiwani humo. Moja ya faida kubwa watakayopata wakazi wa kisiwa hicho cha ziwa Viktoria ni kuwa na huduma ya M-pesa itakayoongeza ufanisi wa biashara na usalama wa fedha za wavuvi.
Wakati serikali ikionesha imani kwa huduma za fedha kupitia simu za mkononi kuwa msaada kwa wananchi wasio na huduma za kibenki huduma ya M-pesa inazidi kuwa tegemeo la wananchi katika kutuma fedha mijini na vijini pamoja na kufanya malipo mbalimbali.
Kwa sasa zaidi ya watanzania milioni tatu na nusu wanatumia mtandao wa huduma ya M-pesa kufanya miamala ya kibishara na ya kijamii milioni nne na nusu kwa siku yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni Moja na hivyo kudhihirisha namna huduma hii ilivyo tegemeo kwa wananchi kwa namna inavyopunguza pengo la ukosefu wa huduma za kibenki nchini.
“M-pesa inawahudumia watanzania wote na imekuwa na faida kubwa kwa kuwapatia huduma rahisi, salama na ya kuaminika hata kule ambako hakuna huduma za kibenki.”Amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza.
“Hakuna mtanzania ambae sasa hafikiwi na huduma za kibenki, kupitia simu yake ya mkononi iliyounganishwa na mtandao wa Vodacom na kusajiliwa ktika huduma ya M-pesa ni kiasi tu cha kupiga *150# anaweza kutuma na kupokea pesa mahali popote nchini, wakati wowote bila kupanga foleni ama kusafiri umbali mrefu.”Aliongeza Meza.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa kampuni ya Vodacom amesema kupitia huduma ya M-pesa maisha yamekuwa rahisi zaidi ambapo mbali na wananchi kutumiana pesa kusaidiana mambo mablimbali ya kifamilia na kijamii ikiwemo michango ya harusi, misiba, ada, matibabu n.k M-pesa imewazesha pia wanannhi kuweza kunua na kulipia huduma kama umeme – LUKU, tiketi za safari, bima n.k.
“Maisha hayakuwa rahisi hivi kabla ya kuanzishwa kwa M-pesa, watu walisafiri umbali mrefu na hata kutumia muda mwingi katika foleni kupata huduma za kutuma na kupokea pesa lakini sasa zaidi ya mawakala wa M-pesa wapatao 40,000 nchi nzima wanawahudumia watanzania usiku na mchana.”
Amesema Meza na kuongeza “Tunachukua kila juhudi kuongeza tija katika huduma za M-pesa ikiwa ni pamoja na kuingia ubia na mabenki pamoja na taasisi za kifedha ili kuyafanya maisha ya watanzania kuwa rahisi zaidi”.
Juzi Niabu Waziri wa Fedha Janet Mbena akijibu swali juu ya ukosefu wa huduma za kibenki na ATM katika baadhi ya maeneo nchini pamoja na maelezo mengine alilieleza Bunge kwamba wakati juhudi za kushawishi mabenki kupanua huduma zao, kwa sasa huduma za fedha kupitia simu za mkononi zinaweza kutumika kupunguza ukubwa wa tatizo.
M-pesa tayari ina ubia wa kibishara na mabenki na taasisi kadhaa za kifedha nchini inayowawezesha wateja wa benki hizo kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao kupitia huduma ya M-pesa bila kufika katika tawi la benki husika.
Huduma ya M-pesa ilianzishwa Aprili, 2008 ikiwa ni huduma ya kwanza nchini ya kutuma na kupokea pesa kutumia simu za mkononi na tangu wakati huo imekuwa ikishuhudia ukuaji wa kasi na kubakia kuwa huduma salama, rahsi, yenye uhakika na ya kuaminika na hivyo kuwa sehemu muhimu ya maisha ya wananchi mijini na vijijini.
No comments:
Post a Comment