Shindano la kumsaka mwanamitindo bora wa kike wa mwaka mwenye kipaji cha kipekee katika sanaa ya mitindo nchini Tanzania limechukua sura mpya baada ya kutangazwa kwa vigezo vya kujiunga na shindano hilo.
Akiongea na Ripota wa Mtaa kwa Mtaa Blog,mkurugenzi wa shindano la unique model Bw.Methudelah Magese amevitaja vigezo hadharani ili wananchi waelewe ni mwanamitindo wa namna gani anaetafutwa ili kuleta maana halisi ya jina la shindano hilo.
Vigezo vya kujiunga na ushiriki wa shindano hilo Pia vigezo vya mshiriki kuwa mshindi lazima akidhi vigezo vifuatavyo na Jumla ya alama ni 100 na zimegawanyika kama ifuatavyo;-
· sura na umbo lenye mvuto wa mwanamitindo. (Alama 30).
· Uwezo wa ziada wa kutembea miondoko ya kimaonyesho ya Mavazi.(Alama 30).
· Uwezo wa kutambua mambo mbalimbali na kujieleza (Alama 20).
· Kujiamini na uchangamfu jukwaani.(Alama 10)
· Nidhamu. (Alama 10)
Jumla ya majaji watatu watakaoteuliwa watapewa semina elekezi na mratibu wa basata namna ya utoaji alama kwa usahihi na kuzingatia haki ya kila mshiriki kwakua shindano hili litakuwa wazi katika kuhakiki haki inatendeka sawa na ubora wa mwanamitindo alivyo , alisema magese.
Hii ni hatua ya kipekee kwa waandaji wa mashindano kuwa wazi namna ya utoaji alama na kumpata mshindi kwakua itatoa mawazo tata na dhana potofu ndani ya vichwa vya wadau wa tasnia ya mitindo.
Wito umetolewa kwa makampuni kujitokeza kudhamini shindano hili ambalo litaleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania ikiwemo kutoa ajira kwa mabinti zetu ambao wanachipukia katika fani hii,pia wabunifu wakubwa kwa wadogo wameombwa kutumia fulsa hii kujitangaza kwa kuwavalisha wanamitindo hao siku ya fainali ambapo inatizamiwa wabunifu wengi kujitokeza.
Pia wanamitindo wote wenye sifa na ndoto zakuwa wanamitindo maarufu kwa kukuza kipaji wameombwa kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 18/11/2012 saa nne asubuhi katika usaili pale Lamada apartments & hotel maeneo ya msimbazi center jijini dar.
Taji la unique model linashikiliwa na mwanamitindo Asia Dachi (anaeonekana pichani) ambapo atalikabidhi kwa mshindi wa mwaka huu 2012 mwishoni wa mwezi disemba.
Unique model 2012 imedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,Mashujaa Investment ltd,Michuzi Blog,Sophernner Investment co ltd,K.d.surelia,Young Don Records,Kiu investment ltd,Oriental bureau de change,,J’s professional ltd,Lamada apartments hotel,T-moto Entertainment,Mtaa Kwa Mtaa Blog,Jiachie Blog,Wajanja Club Blog na Unique Entertainment Blog
No comments:
Post a Comment