Jumuiya
ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya
Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma
na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania.
Jumuiya
hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati,
waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma
na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.
Lengo
la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa
bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya
hao ni Mteja ni Mfalme.
Katika
wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa
katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa
zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.
Ili
kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara
kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara
tu utakapowasilisha kero yako utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika
mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini.
Huduma
Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza
kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la ushindani.
Imetolewa na Mshauri wa
Habari wa Huduma Bongo - hudumabongo@gmail.com
Novemba 9, 2012
No comments:
Post a Comment