HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 20, 2012

TAMPRO NA HELPING HAND ZAENDELEA KUCHANGIA SEKTA YA AFYA TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) Ndg. Sadick Gogo akikabidhi baadhi ya Vifaa Tiba vyenye thamani ya TZS 5 Milioni kwa Muwakilishi wa Taasisi ya Alhalaqul-Islam inayoshughulika na kutoa huduma za Usaidizi katika Hospital Mbali Mbali katika Mikoa tisa nchi. Anayeshuhudia ni Ndg . Sajid Iqbar Mwakilishi wa katika Kanda ya Afrika kutoka taasisi Rafiki ya Kijamii ya  Halping Hand for Relief and Development ya Marekani. 
Wawakilishi wa Taasisi ya Ahlaqul -Islam wakiwa pamoja na Mwakilishi wa Helping Hand na Wanyeji wao wa Taasisi ya Wanajumuia ya Wanataaluma wa Kiislam Tanzania Wakati wa Makabidhiano ya vifaa tiba mbali mbali.
Mwenyekiti wa Halmashauli ya Nzega Mh. Patrick Mbozu pamoja na Mbuge wa Jimbo la Bukene Mh. Selemani Zedi wakisaini Makubaliano ya Ushirikiano na Taasisi ya Helping Hand for Relief and Development pamoja na TAMPRO Kuboresha huduma za Afya katika Halmashauri ya Nzega hususani Jimbo la Bukene. 
Mbunge wa Jimbo la Bukene Mh. Selemani Zedi akifafanua Changamoto na Mafanikio ya Huduma ya Afya katika Halmashauli ya Nzega pamoja na Jimbo la Bukene kwa ofisa mtendaji wa Helping Hand for Relief and Development Africa mbele ya Madiwani wa Halmashauri ya Nzega. Pembeni kulia ni Ndg. Mohamed Kamilagwa, Mkuu wa Idara ya Biashara na Maendeleo ya Jamii ya Jumuia ya wanataaluma wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) Makao Makuu. 
 Mbunge wa Bukene Mh. Zedi Selemani akipokea baadhi ya vifaa tiba vya awali vyenye thamani ya Zaidi TZS 30 Milioni kutoka kwa Muwakilishi wa Africa wa taasisi rafiki ya Jumuia ya wanataaluma wa Kiislam (TAMPRO),  Helping Hand for Relief and Development ya Marekani Ndg Sajid Iqbar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad