Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mheshimiwa Faustin Ndugulile akisikiliza swali toka kwa Muendeshaji wa kipindi cha Makutano kinachorushwa na Kituo cha Radio cha Magic FM,Fina Mango (hayupo pichani).
|
Mheshimiwa Faustine Ndugulile na Fina Mango baada ya kipindi cha Makutano, Magic FM.
Mbunge
wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndungulile amesema kamwe hajawahi
kupinga ujenzi wa mji wa Kigamboni bali alitaka serikali imhakikishie
kuwa wananchi wanashirikishwa katika hatua ya maamuzi juu ya mradi wao.
Mheshimiwa
Ndugulile ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu msimamo wake juu
ya mradi huo katika kipindi cha Makutano, Magic FM. Mradi
huo ambao sasa ni miaka minne tangu uanze kuongelewa umezua mjadala
mkubwa kwa wakazi wa Kigamboni, huku Mhe Ndugulile akitolewa kwenye moja
ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano kutokana na msimamo wake juu
ya mradi huo.
Alisema tatizo la serikali imekuwa haitaki kufuata sheria inayotaka
ushirikishwaji wa wananchi kila hatua katika sera ya mipango miji. Pia
aliongezea kusema wananchi wanataka majibu kuhusu lini mradi utaanza,
wapi utaanzia, nini hatma yao hasa kuhusu fidia.
Alipoulizwa swali na mmoja wa wanakigamboni kuhusu mgogoro uliojitokeza
baina yake na madiwani wa jimbo lake uliosababishwa na wao kutembelea
moja vikao vya bunge kwa mualiko wa waziri wa ardhi na makazi Mhe Anna
Tibaijuka, Ndugulile alijibu kuwa kwa sasa umeisha na kila mmoja
ameshajua kosa lake.
No comments:
Post a Comment