Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International, Balozi Ellen Margarethe akipokea zawadi ya dafu kutoka kwa mkazi wa kijiji cha Jaribu, Wilayani Kisarawe mara baada ya kukagua na kupata repoti za maendeleo za miradi hiyo kijijini hapo, wanaoangalia ni Lydie Boka, ambae pia ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Plan international akifuatiwa na Stella Tungaraza , Mshauri wa masuala ya Kujikimu wa Plan (T), anaeangalia kwa mbali ni Regis Nyamakanga, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Plan Internation.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Plan International, Balozi Ellen Margarethe, akicheza na wananchi wa Kijiji cha Jaribu, Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani, alipowatembelea kwa ajili ya kuangalia na kujifunza utendaji wa miradi inayofadhiliwa na shirika hilo.
No comments:
Post a Comment