Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akijadili jambo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Chrostopher Chiza (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha mpango maalum wa uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga (katikati). Maafisa hao walikua pamoja na kundi la wawekezaji waliokwenda eneo la Gwata, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani leo kuangalia eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya kilimo cha mpunga na miwa chini ya mpango wa SAGCOT.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) akijadili jambo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Chrostopher Chiza (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha mpango maalum wa uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga ndani ya treni ya Tazara leo jijini Dar es Salaam. Maafisa hao walikua pamoja na kundi la wawekezaji waliokwenda eneo la Gwata, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kuangalia eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya kilimo cha mpunga na miwa chini ya mpango wa SAGCOT.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond
Mbilinyi (kushoto) akiwaonyesha wawekezaji watarajiwa ramani ya eneo la
Gwata, wilaya ya Kisarawe lenye ukubwa wa hekta 63,000 lililotengwa kwa
ajili ya kilimo cha mpunga na miwa chini ya mpango maalum wa uendelezaji
kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT). Baadhi ya maafisa
wa serikali na SAGCOT waliwapeleka wawekezaji hao kama moja ya matukio
ya mkutano uliomalizika hivi karibuni Dar es Salaam kuhusu uwekezaji
katika sekta ya kilimo.
No comments:
Post a Comment