Kiongozi wa bendi Mashujaa, Charlz Baba (alieruka juu) akiongoza safu ya ushambuliaji ya Bendi yao hiyo wakati wa Mazoezi kwa ajili ya Uzinduzi wa albam yao ya Pili iitwayo "Risasi Kidole" wakiwa sambamba na Bendi maarufu ya Congo, Wenge BCBG chini ya mwanamuziki nguli JB Mpiana.Shoo ya uzinduzi huo itafanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders club,Kinondoni jijini Dar es Salaa..
Kiongozi wa bendi Mashujaa, Charlz Baba (katikati) akiongoza safu ya
ushambuliaji ya Bendi yao hiyo wakati wa Mazoezi kwa ajili ya Uzinduzi
wa albam yao ya Pili iitwayo "Risasi Kidole" wakiwa sambamba na Bendi
maarufu ya Congo, Wenge BCBG chini ya mwanamuziki nguli JB Mpiana.Shoo
ya uzinduzi huo itafanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders
club,Kinondoni jijini Dar es Salaa.
BENDI ya Mashujaa kesho itazindua albamu yake ya pili ijulikanayo kwa jina la Risasi Kidole pamoja na bendi maarufu ya Congo, Wenge BCBG iliyochini ya mwanamuziki nguli JB Mpiana kwenye viwanja vya Leaders club.
Uzinduzi huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa meneja wa bendi ya Mashujaa, Martin Sospeter.
Sospeter alisema kuwa wamejiandaa vilivyo katika uzinduzi huo na lengo lao kubwa ni kuweka historia katika muziki wa Tanzania.
Alisema kuwa wamekaa kambini kwa muda wa siku mbili na wameandaa vitu vingi vipya kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi nchini. Alisema kuwa kuna rap ya Ua Mbu na Dume la Simba kutoka kwa marapa wao, Saulo Ferguson na Sauti Radi.
Alifafanua kuwa wanamuziki wake wameadhimia ‘kufunika’ katika uzinduzi huo kwani anahistoria nzuri katika muziki wa Tanzania na kufanya kazi katika bendi nyingi.
“Tunawaomba watanzania waje waone nini tunakifanya mbele ya gwiji la muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana, najua wao wamepania, lakini sisi tumepania vilivyo kusafisha nyoyo za mashabiki ambazo kwa sku nyingi hawajapata burudisha la mioyo zao,” alisema.
Kiongozi wa bendi hiyo, Charlz Baba alisema kuwa wamepania kutoa somo kwa wanamuziki wa dansi hapa nchini ambao wamekuwa wakisubiri waone watafanya nini. Alisema kuwa wameandaa nyimbo nyingi nzuri na wamepatia kutawala soko la muziki hapa nchini.
“Njooni muone nini tunafanya katika muziki wa dansi, kambi yetu imekuwa nzuri na mafanikio makubwa, naomba mashabiki waje kutuunga mkono nasi tutawaunga mkono kwa kutoa burudani safi,”alisema Chalz.
Albamu ya Risasi Kidole ina jumla ya nyimbo sita. Nyimbo hizo ni Umeninyima, Tikisika, Hukumu ya Mnafiki, Ungenieleza, Kwa Mkweo na wimbo uliobebab jina la albamu hiyo, Risasi Kidole.
No comments:
Post a Comment