Mgonjwa
Stella Samuel Mwita mwenye umri wa miaka 32 amefariki dunia Novemba
2, 2012 saa 12 asubuhi katika Idara ya Magonjwa ya Akili Hospitali ya
Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa toka Septemba 2012.
Stella
alikuja Dar es Salaam kutokea Mtwara miaka mingi iliyopita na wakati wa
ugonjwa wake hakupata kutembelewa na ndugu yeyote yule.
Shughuli za mazishi zinasubiri ndugu wa marehemu. Mungu ailaze roho yake pema peponi.
|
Imetoloewa na;
Aminiel Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Hospitali ya Taifa Muhimbili
No comments:
Post a Comment