Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh. Peter Kallaghe leo ameitisha mkutano kati yake na maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na maafisa wa Ubalozi ili kuzungumza nao na kupata taarifa muhimu juu ya maadandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM), yanayotarajiwa kuanza siku ya jumatatu Novema 5 mpaka Novemba 8 mwaka huu katika jiji la London.
Maonyesho ya Utalii ya (WTM) yanayoandaliwa nchini Uingereza ni maonyesho makubwa na yanashirikisha makampuni kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa ajili ya kuuza bidhaa zao, hasa Mahoteli, Makampuni ya Ndege na makampuni ya Utalii, Mwaka huu Tanzania inashirikisha makampuni zaidi ya 55 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Katika picha juu akisisitiza jambo katika mkutano huo, wakati wa mkutano huo ambapo aliza kila jambo ambalo linahitaji kupata majwabu muhimu kabla ya kuanza kwa maonyesho hayo.
Maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakimsikiliza kwa makini Mh. Balozi Peter Kallaghe wakati akiongea nao katika mkutano huo
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akifafanua jambo katika mkutano huo, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi.
Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) akimfafanulia jambo Mh. Balozi Peter Kallaghe wakati wa mkutano huo katika ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Siku zote ukitaka kufikia malengo yako unatakiwa kuwa na mfano wa kufananisha na kujua kweli unasonga kwa jinsi utalii wetu unavyoendeshwa kwa sasa ni ngumu sana kujua hali halisi bila kufanya research za kutosha na kuwa na strategic plan za tourism ili twende mbele,wenzetu wa Brazil wameanzisha wizara ya utalii toka 2003 leo hii wamefikia malengo ya juu na ni sekta ya tatu kwa kuingiza pesa kwa taifa,wameweza kuwa na kitu kimoja chenye kuboresha utalii kila siku na kinachoendelea nyumbani ni kuingiliana kazi kwa sekta zinazofanana,na wa Brazil wana ofisi za utalii ktk nchi ambazo raia wake ni wapenzi wa kutembelea nchi yao kwa lengo la kushawish wasiofika(road show)sio kutegemea maonyesho ambayo wengi wa maofisa wanakuja kutembea na sio kufanya kazi.Na Elimu ya utalii iwe kipaumbele kwa maofisa sio mambo ya kujuana tu.
ReplyDeleteWizara ya utalii na maliasili sio sawa hata kidogo,utalii kama kweli tunalengo zuri la kuboresha na kuwa msatari wa mbele tunapaswa kuwa na wizara ya utalii tu na maliasili iamishiwe kwenye nishati na madini.Muheshimiwa Rais pls fanya maboresho ili kuleta tija ya utalii nchini,kilichopo sasa ni kizungulumkuti,TTB,Tanapa,na other bodies zinatakiwa kuwa chini ya mwamvuli mmoja ktk kutangaza utalii nje ya nchi na sio kama sasa kila mmoja anatangaza kwa muda na picha zake,its wrong,image ya Tz iwe mmoja yenye lengo la kuvutia watalii
ReplyDelete