HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 29, 2012

Naibu Waziri wa Uchukuzi afanya ziara Katika Uwanja wa Ndege wa Julisu Nyerere

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA),wakati alipofanya ziara katika Kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Leo,kujionea shughuli Mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri wa Uchukuzi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi. Suleiman Suleiman.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(mwenye suti nyeusi) akiangalia eneo la Kipunguni B ambalo lilifanyiwa tathmini kwa ajili ya kuongeza eneo la Kiwanja cha Ndege cha Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata maelezo ya namna kituo cha hali ya Hewa kinavyofanya kazi katika utoaji wa Taarifa mbalimbali za hali ya Hewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kutoka kwa Bi. Pamela Gabriel kutoka Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA).Naibu Waziri wa Uchukuzi alifanya Ziara hiyo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Uwanja huo leo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata malezo kutoka kwa Afisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Bw. Elieza Mwalutende, wakati Naibu Waziri huyo alipotemmbelea Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl . Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanja hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(aliyeweka mikono miwili mfukoni) akipata maelezo ya namna kikosi cha zima Moto katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere kinavyofanya kazi,Wakati wa Ziara yake hii leo Katika uwanja Huo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(aliyeweka mkono mfukoni) akipata maelezo ya namna Genereta za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzani(TAA) zinavyofanywa kazi endapo umeme utakatika kutoka kwa Bi. Rehema Ahmed (mwenye Hijabu), wakati wa Ziara yake katika uwanja huo leo.
Hayo ni Majenereta yanayotumika endapo Umeme wa TANESCO unapokatika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijjini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege(TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman, akisisitiza jambo wakati Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(aliyejishika Kichwa), alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Uchukuzi, Bw. I. Nchasi.
Naibu waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba ,akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA),alipokutana nao leo jijini Dar es Salaam, katika Ziara yake ya kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa katika Uwanja wa Mwl Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(wa nane kutoka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara ya Uchukuzi. Naibu Waziri wa Uchukuzi amefanya Ziara katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kujionea shughuli mbalimbali zinazonafaywa katika Uwanja huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad