HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 21, 2012

Mwanaanga wa Kwanza kutoka Barani Afrika kwenda Mwezini atoa somo wa Wanafunzi wa Shule za Sekondari jijini Dar

 Mwanaanga wa Kwanza kutoka Barani Afrika kwenda Mwezini ambaye ni Mzaliwa wa Nchini Cameroon,Patrick Baudry akifafanua jambo kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari za Jijini Dar es Salaam na Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati akitoa mafunzo juu ya Safari nzima ya kwenda kwenye Mwezi na kurudi Duniani,katika Semina iliyofanyika mapema leo kwenye Ukumbi wa Nkurumah,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Semina hii ni Maalum kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari nchini ambao watashindana na Wanafunzi wenzao kutoka nchi zote za Afrika kwenye Shindano kubwa la kuandika NSHA na Kuchora Picha,ambapo mshindi atapata nafasi ya kwenda jijini Paris Ufaransa kujionea namna Safari ya kwenda kwenye Mwezi inavyokuwa.Shindano hilo linaratibiwa na Eutelsat na Kudhaminiwa na DSTV.
Meneja Mahusiano wa Multchoice Tanzania, Barbara Kambogi akitoa maelezo machache kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa Makini Mada mbali mbali zilitokuwa zikitolewa ukumbini hapo.
Mwanaanga wa Kwanza kutoka Barani Afrika kwenda Mwezini ambaye ni Mzaliwa wa Nchini Cameroon,Patrick Baudry akisaini kwenye Vitabu vya wanafunzi hao mara baada ya kumaliza kutoa Mafunzo mbalimbali ya namna watu wanavyofanya safari ya kwenda Mwenzini.
Mwanaanga wa Kwanza kutoka Barani Afrika kwenda Mwezini ambaye ni Mzaliwa wa Nchini Cameroon,Patrick Baudry akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya ujio wake hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad