Mkurugenzi
wa Kampuni Mpya ya QS Muhonda J Entertainment, Joseph Muhonga (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es
Salaam leo wakati akitangaza uzinduzi wa Kampuni yake hiyo na Kutangaza
ujio wa Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo,JB Mpiana ambaye
atatumbuiza katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam Novemba
30.Katika onyesho hilo ambalo litasindikizwa na wanamuziki mbali mbali
hapa nchini wakiwemo,H-Baba,MB Dog na Ney wa Mitego ambao wapo chini ya
lebo ya Kampuni hiyo pia kutafanyika uzinduzi rasmi wa Albamu mpya ya
Bendi ya Mashujaa uitwao "Risasi Kidole" .
Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,MB Dog kulia na H-Baba.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Hamis Ramadhan a.k.a H-Baba (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam
leo juu ya maandalizi yake ya kufanya shoo jukwaa moja na Mwanamuziki
wa Kimataifa kutoka nchini Congo,JB Mpiana ambaye
atatumbuiza katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam Novemba 30.
No comments:
Post a Comment