Kwa mujibu wa tafsiri ya neno uchafu ni kitu chochote kisichokuwa kwenye mpangilio maalum au utaratibu unaokubalika, angalia vizuri ukaaji wa haya mabango.
Na hapa napo ndio vile vile viongozi wa
Ukerewe jipangeni kwa hili, ingawa kila mmoja anajicho lake lakini
lakwangu limeona hli silo labda wenyewe.
Hili nalo sijui ni gofu au nini sijui lakini kuwepo kati ya mji wa Nansio halifurahishi.
Hii ndioyo Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe ambapo hivi karibuni wamefanikiwa kuzindua majengo mapya kadhaa.
Majengo ya zamani ambayo yanaonekana yakiwa imara hadi leo kutokana na kutunzwa vizuri.
Moja ya matunda yaliyopo kwa sasa
Wilayani humo ni embe ambazo zipo nyingi sana lakini mbali na embe
mananasi nayo yameanza kuvunwa.
Hii ni alama ya Ukerewe ipo kwenye kituo cha mabasi kilichopo Nansio.
Majengo ya Halmashauri ya Wilaya ya
Ukerewe yanavutia kutokana utunzwaji wake pamoja na kuwa ya miaka mingi
bado yapo kwenye mwonekano nzuri.
Na huu ni moja ya mitaa ya Nansio, mtaa huu ukijulikana kama Musoma Road.
ni jukumu la vionguzi kusema kweli kuiweka ukerewe hali inayoleta matumaini kama sehem zenye historia kubwa nchini
ReplyDelete