Kutokana na Ziwa Victoria kuwa na visiwa
vingi usafiri wa aina hii hutumika zaidi kusafirisha abiria, kituko
kwenye usafiri huo ni kwamba unafungwa mziki hata ikiwa umbali wa mita
miatatu kutoka ufukweni unausikia baada ya kufungwa vipaza sauti
vinavyotumika sana misikitini.
Mmoja wa kina mama wa Musoma akiwa
kazini na mkokoteni wake, kina mama wengi wa wilaya hiyo wamekua
wakijishughulisha na kazi mbalimbali ambazo kwenye jamii nyengine
zinaonekana kama kazi za wanaume pekee.
Kando ya barabara kuu ya kuingia Musoma Mjini karibu na Stendi ya mabasi ya zamani.
Eneo la kupandia kivuko cha MV Musoma kuelekea maeneo ya Kilese Tarime
likiwa halina kizuizi chochote cha magari, ambapo ni hatari kwa usalama
wa watu na magari yanayoelekea kwenye sehemu hiyo.
Mitaa ya Musoma Mjini.
No comments:
Post a Comment