Hapa ni katikati ya jiji pakiwa na bustani zinazovutia Mbele
ya Mtaa Kemondo ikilipamba jiji hilo.
Kama majiji yote yangekuwa na vifaa kama hivi kila kwenye
nguzi ya taa kama ilivyo jijini Mwanza basi suala la usafi wa Mazingira kwenye
majiji yetu lingekuwa lakujivunio kuliko ilivyo sasa.
Hata mtu anaefanya usafi mwenyewe hufanana na usafi husika
tofauti kabisa na majiji mengine huyo anaefanya usafi mwenyewe mchafu kweli
atafanya usafi? Ipo haja ya majiji mengine kuja kujifunza haya.
Kamera yatu ilifika hadi kwenye eneo la Soko kuu na kukuta
gari la kisasa la kuzolea taka likiendelea na kazi na kwamujibu wa watu
walizozungumza na MTAA KWA MTAA, kazi hiyo hufanywa kila siku. Kama ilivyo kwa
jiji la Dar es Salaam wafanyabiashara hupanga biashara zao hadi sehemu za
takatata hizi ni baadhi ya Changamoto zinazotakiwa kufanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment