Hawa jamaa ninavyowafahamu ni wadau wa
zuri wa mazingira na hisi hata hapa wanafanya kazihiyo ndio maana
nirafiki wa binadamu hawabughudhiwi.
Mrundikano wa vyombo vya ziwani
vilivyoharibika huchafua mandhari ya eneo la Mwaloni ambapo panapirika
nyingi za kushusha na kupakia mizigo pamoja na biashara za aina
mbalimbali unaleta mazingira ya uchafu na si taswira nzuri kwa jiji
lenye sifa ya usafi wahusika waliangalie hili.
Hapo hapo Mwaloni kamera ya raha za pwani ikamulika mtoto huyu akijaza maji kwenye chupa kwenye chemba ya maji taka hata hivyo hakuweza kunieleza anayafanyia nini maji haya.
Taswira pekee ya shena ya kuni
itakuonyesha namna misitu yetu inavyoteseka huko porini, bila kupata
shida ukifika tu kwenye eneo la Mwaloni unapokewa na shehena hii ya
kuni.
Soko lenyewe la mwaloni ni hili huku biashara kubwa kwenye eneo hilo ikiwa ni samaki na ndizi ingawa na biashara nyingine za aina mbalimbali zinafanyika.
No comments:
Post a Comment